Eda ya mwanamke ambaye
Question
Je, ni muda gani wa eda kwa mwanamke ambaye mumewe amefariki? Je, inajuzu kwake kutoka nje ya nyumba yake wakati wa eda?
Answer
Muda wa eda kwa mwanamke ambaye mumewe amefariki ni miezi minne na siku kumi za Hijria. Kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi} [Al-Baqarah: 234].
Inajuzu kwake kutoka nje nyumbani kwa mumewe wakati wa mchana, kwa kuzingatia kulala usiku katika nyumba ya ndoa siku zote za eda.
Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.