Athari za uvumi kwa jamii
Question
Je, ni nini wajibu wa Muislamu kwa uvumi unaozushwa karibu naye?
Answer
Uislamu ulikausha vyanzo vya uvumi kwa kuwalazimisha Waislamu kuzichunguze habari kabla ya kuegemeza hukumu juu yake, na kuamuru mambo yapelekwe kwa watu wake na kufahamu kabla ya kuzitangaza na kuzizungumzia. Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.} (Al-Hujurat: 6).
Uislamu pia umekataza kusikia na kueneza uvumi, na Mola Mtukufu amewatahadharisha wale waenezao uvumi na fitna. Mwenyezi Mungu amesema: {Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu} [At-Tawbah: 47].