Adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa Magaidi
Question
Ni ipi adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa Magaidi?
Answer
Mwenyezi Mungu Anasema: {Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.60. Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa. 61. Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.} [AL-AH'ZAB 60-63].
Wafasiri wamesema: MURJIFUUNA ni wale ambao wanahofisha watu na kueneza hofu na woga kati ya watu kwa batili; na wanafanya hivyo kwa malengo yao duni, kisha Mwenyezi Mungu Akataja idadi kadhaa ya adahabu zitakazowapata kwa kutotubia kwao na kuacha vitendo hivi viovu.
Adhabu ya kwanza ni kuwafedhehesha; nayo ni kuwasalitisha juu yao, na ya pili ni kuwafukuza katika jamii wanazoishi, na ya tatu ni laana; nayo ni kufukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, na ya nne ni kuuwawa kwa watakaoshika silaha katika wao; nayo ni amri ya kuwapiga Jihadi. Kisha Mwenyezi Mungu Akabainisha kwamba adhabu hizi kwa mfano wa watu hawa katika mataifa mbalimbali ni desturi yake ambayo haibadiliki wala haifutwi.