Kuwasomesha wasichana
Question
Nini hukumu ya kuwazuia wazazi au mmoja wao kumsomesha bintiye?
Answer
Uislamu uliomba na kuhimiza kutafuta elimu, na uliweka hadhi ya watafutaji wake juu kabisa katika matini nyingi, na hakuna tofauti katika hilo baina ya mwanamume na mwanamke. Matini za Sharia Tukufu hazikutofautisha baina ya mwanamume na mwanamke katika kuhimiza kutafuta elimu, kama kwamba haja ya mwanamke kwa elimu ni sawa sawa na haja ya mwanamume, na kupuuzwa kwa baba katika kuwasomesha watoto wao wa kike - kwa kuwazuia kuhudhuria shule au kuwafukuza kutoka shule - ni kunyimwa haki hii ya asili.