Kukwamisha masilahi ya watu.
Question
Ipi hukumu ya kutofanya kazi rasmi kwa kufanya kazi binafsi?
Answer
Mfanya kazi ni mwenye kuaminiwa kwenye kazi ambayo ameajiriwa nayo, wala haifai kwake kuacha na kushuhurishwa na kazi binafsi, isipokuwa ikiwa kuna makubaliano katika mkataba au kuwa ni jambo la kawaida, ikiwa mfanya kazi atatumia wakati wa kazi kufanya mambo yasiyokuwepo kwenye makubaliano basi anakuwa ni amekiuka makubaliano yake, Kisharia na kisheria anastahiki makosa na adhabu.