Uislamu umetahadharisha kutokana na...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uislamu umetahadharisha kutokana na ukufurushaji

Question

Kwa njia gani Uislamu umetahadharisha kutokana na ukufurushaji?

Answer

Kwa hakika kuwahukumu watu ukafiri ni fitina kubwa na hatari inayotishia umma wa kiislamu, na kusababishia Waislamu wasambaratike na kugawanyika, bali hatari ya fitina hii inasababisha kupuuza uharamu wa umwagaji damu na kupoteza haki, amani na usalama katika jamii, kwa hiyo, Uislamu umetoa tahadhari kali kutokana na  fitina hiyo, ambapo Mwenyezi Mungu Amesema: "wala msimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii" [An-Nisa'a: 94], pia Sharia ya kiislamu inamtahadharisha Muislamu asimshutumu Muislamu mwenzake kwa ukafiri kwani anayefanye hivyo pasipo na haki, basi huwa sawa sawa na kafiri, Mtume (S.A.W.) amesema: "Yeyote anayemwita Muislamu mwenzake Kafiri, basi mmoja wao huwa ndiye kafiri". Zaidi ya hayo, Mtume akaeleza kuwa kumtuhumu Muislamu kwa ukafiri ni sawa na kumuua kwani hatari ya mambo haya mawili ni kubwa mno, Mtume amesema: "Yeyote anayemlaani muumini kuwa ni kafiri huwa ni sawa sawa na kumua" (Hadithi mbili zimesimuliwa na Al-Bukhary), aidha Mtume (S.A.W.) alitoa tahadhari kali kutokana na fitina hiyo ya kumlaani muumini kwa ukafiri au ufuska, akisema: "Haijuzu kwa mtu amlaani mwingine kwa ufuska, wala kumtuhumu kwa ukafiri, kwani anayefanya hivyo huwa anajisababisha kujipatia laana hizo endapo mwenzake huyo hakuwa hivyo" (Imesimuliwa na Al-Bukhary), kijumla, yeyote anayewakufurisha wenzake huwa anajikurubisha na  moto, Mwenyezi Mungu Atukinge nao.

Share this:

Related Fatwas