Hatari ya Ukufurishaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Hatari ya Ukufurishaji

Question

Ni nini hatari ya kukufurisha jamii? Na je, kuhukumu jamii kwa ukafiri ni jukumu la watu wa kawaida?

Answer

Kwa hakika ukufurishaji au kuwahukumu wengine kwa ukafiri ni miongoni mwa maovu yaliyoathiri vibaya jamii na kusababisha zisambaratike, na kutokea machafuko makubwa mpaka umwagaji damu pasipo na haki, ilhali sheria ya kiislamu ilisisitiza hatari ya tabia hii na kuikataza katika Qur`ani Takatifu na Sunna za Mtume, Mwenyezi Mungu Amesema: "wala msimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe si Muumini" [An-Nisaa: 94], naye Mtume (S.A.W.) amesema katika Hadithi: "Yeyote anayemhukumu mwenzake kwa ufuska au ukafiri hurudi juu yake endapo mwenzake hakuwa hivyo" [Imesimuliwa na Al-Bukhary], pia Mtume amesema katika Hadithi nyingine: "Mambo matatu ni miongoni mwa misingi ya Imani; kutomuudhi anaye kiri kuwa hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, kutomhukumu ukafiri kwa dhambi, wala kutomhukumu kutoka katika Uislamu kwa kitendo fulani" [Imesimuliwa na Abu Dawood], kwa hiyo, wanavyuoni wa Umma walikubaliana kuwa kumkufurisha Muislamu yeyote hakuzingatiwa isipokuwa kwa mujibu wa hukumu ya kadhi siyo kwa maoni ya watu wa kawaida, na kwamba Muislamu anapaswa kujitahadhari asimhukumu yeyote katika Waislamu wanaowajibika Swala kwani hukumu hiyo ni hatari sana, ambapo jambo hilo huenda likasababisha umwagaji damu za watu na kupoteza haki na kinga zao kwa kuwahukumu kutoka katika Uislamu.

Share this:

Related Fatwas