Umuhimu wa kufanya jitahada kwa pamoja
Question
Ni upi umuhimu wa kufanya jitihada kwa pamoja na katika makundi kwa maisha yetu ya kisasa?
Answer
Kufanya jitihada kwa pamoja na katika makundi ni jambo lenye umuhimu mkubwa hasa katika enzi yetu ya kisasa kwa lengo la kufikia masuluhisho ya masuala ya kijamii ya kisasa, kwani jitihada za mtu mmoja binafsi ni ngumu kulingana na maendeleo makubwa endelevu na ya haraka ya mifumo ya maisha na matukio yake, jambo linalohitaji jitihada kubwa na za kina zaidi kwa ajili ya kuvuka changamoto za kila siku kwa namna inavyoendana na mabadiliko ya enzi, kwa hiyo, hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya hayo peke yake, kwani ni ngumu kupatikana mmoja anayetambua masuala yote ya jamii yake ingawa anajitahidi sana hasa katika siku hizi ambapo eneo la nchi za kiislamu limepanuka sana na idadi ya Waislamu inaongezeka katika nchi mbalimbali duniani, hivyo, jitihada hupaswa kufanywa kwa pamoja na ndani ya makundi au asasi maalumu zinazoweza kuenda sambamba na maendeleo hayo, pia, jitihada za pamoja husaidia kuimarisha mazungumzo na kushauriana katika masuala ya kitaaluma na kuomba msaada wa wataalamu wazoefu katika nyanja tofauti, hasa katika enzi ya kushughulikia fani au taaaluma maalumu, tukitambua kuwa ni ngumu kwa mtafiti mmoja awe na ujuzi wa taaluma, tamaduni na fani mbalimbali zinazokua kila siku. Kwa hivyo, kufanya jitihada kwa pamoja ni aina ya makubaliano ya pamoja na ni njia ya kuishi pamoja na kusameheana kifikra na sababu kubwa ya kuunganisha umma wa kiislamu.