Kusoma Qurani kwa pamoja

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Qurani kwa pamoja

Question

Ni ipi hukumu ya kusoma Qurani kwa pamoja?

Answer

Kusoma Qurani kwa pamoja kwa nidhamu ambako hakuna muingiliano wala ushawishi wakati wa kusoma au kujifunza - kama ilivyozoeleka katika katika darsa za Qurani Tukufu katika baadhi ya misikiti na madrasa- kunajuzu kisharia, nayo ni katika dhikri za pamoja ambazo mwenye kufanya anapata thawabu nakufikia malengo ya kufundisha Qurani.

Imepokewa kutoka kwa mtume S.A.W. kuandaa darsa za Qurani kwa namna ambayo hakuna ushawishi kwa yeyote kwa mwingine; kama ilivyokuja katika Hadithi ya Abou Hazm al-tamar kutoka kwa Albayadhy R.A. kwamba Mtume S.A.W. aliwakuta watu wakiwa wanasali wakisoma Qurani kwa sauti, akasema: “hakika anayesali anamuomba Mola wake, basi aangalie anachokiomba, wala msisomeane Qurani kwa sauti” hadthi hii imepokelewa na Imamu Malik katika Muwataa.

Share this:

Related Fatwas