Maana ya kufuru na Imani
Question
Kufuru ni nini? Na ni nani mwenye mamlaka ya kuwahukumu watu kwa kufuru au imani?
Answer
Kwa hakika Uislamu umekuja kwa ajili ya kuwaongoza watu kwenye njia iliyonyooka na kuwatoa katika upotofu kwenda uongofu, ukakubaliwa na watu na kukataliwa na wengine, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani} [Al-Baqarah: 257], basi wale walioukubali dini hiyo ni waumini, na walioukataa wakiwa na kiburi na jeuri ndio makafiri, hivyo, kufuru katika lugha ni kufunika na kuficha, mfano wake: tunasema: amekufuru neema; kwa maana ya kuificha na kuikana, na kufuru ni kinyume na imani, na kufuru ni: Kukana neema kwa maana ya kinyume cha shukurani, inasemwa kuwa: Mtu amekufuru kwa kitu hicho kwa maana ya: kukikana, pia, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu} [Ibrahim: 22], pia neno la kumkufurisha humaanisha kumhukumu ukafiri.
Kwa mtazamo wa sheria, ukafiri ni: kukana yaliyojulikana katika dini ya Mtume wetu Mohammed (S.A.W.) kama vile kukana na kukataa kuwepo kwa Muumbaji wa ulimwengu na kukataa ujumbe wa Mtume, kukataa nguzo za Uislamu na kuhalalisha yaliyoharamishwa kwa dalili thabiti n.k.
Ukufurishaji ni hukumu ya sheria ambayo hutolewa kwa kila mwenye sifa za kukufurishwa na maagizo ya sheria na makatazo yake, basi kutoa hukumu hiyo ni jukumu la Mufti na Kadhi, hakuna mtu isipokuwa Mufti au Kadhi anaye haki ya kuwahukumu watu kwa ukafiri, Imamu Al-Sobky amesema: "Ukufurishaji ni hukumu ya Sharia ambayo hutolewa kwa sababu ya kukana uungu au upweke au ujumbe au kusema kauli au kufanya kitendo ambacho Sharia imepitisha kuwa ni ukafiri wazi hata ikiwa si kwa njia ya kukana na kukataa"