Hakimiya

Egypt's Dar Al-Ifta

Hakimiya

Question

Makundi ya kigaidi na wenye fikra potofu wanadai kuwa Waislamu hawakutegemea sharia ya Mwenyezi Mungu na badala yake wakategemea sheria za kikafiri zilizotungwa na makafiri, je, madai haya yako sahihi?

Answer

Kwa ufupi, hakimiya inamaanisha kuwa watu kurejelea sharia ya Mwenyezi Mungu katika masuala yote ya dini na dunia.

Hapana shaka kuwa kurejelea sharia ya Mwenyezi Mungu katika hukumu ni wajibu na ni jambo la msingi, na ni faradhi juu ya Waislamu wote wakiwa wameridhika kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote.

Kila anayekiri kuwa sharia ya kiislamu ni chanzo cha sheria na hakukana lolote kati ya mambo ya msingi kama vile; faradhi ya Swala, Zaka na uharamu wa ulevi na wizi kwa mfano, basi huwa mbali na makafiri wakati haisihi kutuhumiwa kuwa ni kafiri.

Kutoa hukumu ya kijumla kwa kuwakufurisha watu waliorejelea sharia zilizotungwa kwa kurejelea sharia isiyokuwa ya Mwenyezi Mung ni maoni ya Khawariji na waliowaunga mkono miongoni mwa wanaowakufurisha Waislamu kiholela kwa dhana na matamnio yao wenyewe, lakini lililotakiwa kusisitizwa ni kwamba sheria zote zilizotungwa na kuandikwa na kutekelezwa katika nchi za kiarabu na kiislamu kwa ajili ya kupitishwa katika mahakama ya sheria na kienyeji – kwa yakini – ni sheria ambazo zilitokana na maoni yaliyozingatiwa na Wanachuoni na Maimamu wa Fiqhi au baadhi ya maoni katika madhehebu, ingawa maoni haya yasingekuwa na uzito sana, pia, baadhi ya sheria zilitungwa na kupitishwa baada ya kuhakikisha kuwa hazipingani na matini za sharia na kuwa zinaambatana na manufaa ya umma.

Share this:

Related Fatwas