Utengezaji wa misimamo mikali.
Question
Namna gani huzalishwa akili za misimamo mikali katika jamii?
Answer
Uzalishaji wa misimamo mikali siku zote hauendi kwenye mtindo mmoja, kwani kutengeneza misimamo mikali na haiba ya muumini jambo gumu, linafungamana na sababu nyingi za nje zinazohusu muundo wa kijamii na mabadiliko yake pamoja na hali zake za sasa ambazo zinazingatiwa ni mazingira yanayokubali, na kwa sababu zingine zinazohusu sifa za mtu mwenyewe wa msimamo mkali pamoja na muundo wake kisaikolojia, nayo ni vihamasishi vya msimamo mkali, katika wigo wa hizo sababu hukamilika kazi za mabadiliko na muelekeo kwenye msimamo mkali, na kutengeneza mtu muumini wa kufuata matumizi ya nguvu na mapambano.
Ambalo linapaswa kuzingatiwa ni upande wa kimaarifa katika kuzalisha haiba ya msimamo mkali ni muunganiko dhaifu na wenye athari ndogo zaidi katika kuunda na kutengeneza msimamo mkali, na wala sio kusudio la hilo kupunguza nafasi ya vitabu mitandao na chaneli za kuangaliwa fikra za misimamo mikali, lakini kusudio ni kusisitiza kuwa vyanzo hivyo vya maarifa ndio njia ya kutawala akili, hujaribu kutumia mambo na misikumo ya kijamii na kinafsi kwa mtu ili kuchukuwa nafasi yake katika utamaduni wake na akili yake, na kufanyia kazi fikra zake na mtazamo wake kuchukuwa nafasi za fikra zote na misingi ambayo mtu alikuwa anafuata na kuamini, kisha vyanzo hivyo nguvu yake inategemea na maandalizi ya mtu na kukubali kwake kuelekea kwenye mitazamo mikali.
Huenda dalili ya hilo ni kuwa vyanzo hivyo vya kimaarifa bado vinavuta sehemu ndogo ya upande wa raia, bado wengi wenye sifa ya matumizi mazuri ya akili wanaelekea kwenye fikra za kati na kati na usawa.