Motisha za kisaikolojia kwa watu wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Motisha za kisaikolojia kwa watu wa misimamo mikali (4)

Question

Ipi athari ya kukimbilia kihisia na mielekeo ya kujitenga kwa mtu wa msimamo mkali?

Answer

Kukimbilia hisia kunakusudiwa kuzidisha jazba, ni sawa sawa ikiwa jazba ya kupenda au kuchukia au kukasirika, mtu mwenye kukimbilia kwenye hisia hawezi kuwa wa kati na kati na kuchukuwa misimamo ya usawa na iliyokomaa kuelekea msimamo wake wa kimaisha, na hisia zake ambazo anahisi kwa upande wa watu, hivyo upendo unaweza kumsukuma mtu mwenye sifa ya kukimbilia hisia kwenda kwenye misimamo mikali kwa kuwepo tu mtu katika safu za watu wa misimamo mikali mtu anayempenda, hivyo huelekea kwao na kujiunga kwenye matendo yao kwa kufungamana kwake tu na huyo mtu, na kinyume chake kwani kumchukia mtu au kikundi fulani kunaweza pelekea kufanya jambo hilo hilo, na kukubaliana na fkra yeyote ile au kikundi chochote kile kunaweza pelekea vitendo vyao kuwa kero kwa huyo mtu au kikundi, ndio hivyo hivyo mgongano wa hisia na kuzidisha katika majibu kunaweza kumalizikia kwa mtu kuwa na msimamo mkali.

Ama mielekeo ya kujitenga watu wengi wanaojifunza wanaona kuwa mtu wa msimamo mkali anaweza kwa sehemu kubwa anaweza kuwa na hali ya kujitegemea na kuwa mbali na watu wengine, isipokuwa kuna uhusiano kati ya kujitenga na msimamo mkali kwa upande mmoja, kwa sababu vikundi vya misimamo mikali mara nyingi hutumia maelezo machache yanayopelekea mtu kuchukuwa uamuzi wa peke yake, nao ni pacha na asili ya mtu wa kujitenga ambaye hupendelea fikra hizi na kuhisi imani kwa hao watu, jambo linalomfanya kwa sehemu kubwa kujiunga na kufuata fikra hizo za msimamo mkali. 

Share this:

Related Fatwas