Kutembelea Mawalii na waja wema
Question
Je! Inafaa kutembelea makaburi ya waja wema?
Answer
Kutembelea makaburi kwa ujumla ni jambo la Kisharia kwa wanaume na wanawake, pindi jambo linapokuwa la Kisharia basi linapendeza zaidi linapohusishwa na Manabii au waja wema katika Umma wa Mtume S.A.W. kama vile kutembelea makaburi ya watu wa nyumbani kwa Mtume Wanachuoni na Mawalii, dalili ya hilo kauli ya Mtume S.A.W.:
“Hakika yangu niliwakatazeni kutembelea makaburi basi yatembeleeni kwani yenyewe yanawakumbusha Akhera”. Hadithi imepokewa na Imamu Muslim.
Na katika mapokezi mengine Mtume S.A.W. anasema:
“Nilikuwa nimewakatazeni mambo matatu: Kutembelea makaburi basi yatembeleeni, kwani kuyatembelea ni mawaidha na mazingatio”. Hadithi Imepokewa na Imamu Ahmad.
Ikiwa asili ya kutembelea kaburi ni jambo la Kisharia basi kuliendea ni jambo la Kisharia pia, ama kauli yake Mtume S.A.W.:
“Haifungwi safari isipokuwa kwenye Misikiti Mitatu: Msikiti Mtakatifu wa Makka, Msikiti wa Mtume S.A.W na Msikiti wa Al-Aqsaa”. Hadithi Imekubaliwa na Wanachuoni wote wa Hadithi.
Kilichohusishwa kwenye Hadithi ni kutembelea Misikiti na wala si makaburi, kwa mfano wala humuoni mtu anayesema: Mimi ninasafiri ili kutembelea Msikiti wa Imamu Hussein Amani ya Mungu iwe kwake, au kutembelea Msikiti wa Sheikh Shadhiliy Rehma za Mungu ziwe kwake, bali makusudio yao ni kumtembelea Mja mwema kwenye kaburi lake, nalo ni jambo linalofaa Kisharia.