Kutekeleza Hijja na Umrah kwa malip...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutekeleza Hijja na Umrah kwa malipo ya awamu

Question

Ni ipi hukumu ya kuhiji na kutekeleza Umra kwa malipo ya awamu?

Answer

Imethibitika kisheria kwamba umiliki wa gharama za Hijja au Umra - ambazo zimeelezwa katika Fiqhi kwa maandalizi na Kipando - ni sharti tu la wajibu na si sharti la kusihi Hija. Maana yake ni kwamba hali ya  kutoimiliki maandalizi na kipando wakati wa kuhiji haimaanishi kuwa Hijja si sahihi, bali ina maana ya kuwa si wajibu kwake, ili asipohiji wakati huo, hakuna dhambi juu yake, lakini akiingia katika Ihram kwa ajili ya Hijja ni wajibu kuikamilisha, na Hijja yake ni sahihi, na Hijja ya faradhi imeondolewa kwake, na hali kadhalika katika Umra.

Kwa kuzingatia hapo juu: Hijja na Umrah kwa malipo ya awamu ni halali kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.

Share this:

Related Fatwas