Kusoma Basmala kwa sauti mwanzoni m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Basmala kwa sauti mwanzoni mwa sura ya Al-Fatiha katika Swala

Question

Ni ipi hukumu ya kusoma Basmala kwa sauti mwanzoni mwa Sura ya Al-Fatiha katika Swala? 

Answer

Kusoma Basmala kwa sauti mwanzoni mwa Suratul-Fatiha katika Swala ni miongoni mwa masuala yenye maoni tofauti tofauti ya Wanachuoni, ambapo wafuasi wa Madhehebu ya  Imamu Shafi na kundi la wanavyuoni wengine wanaona kuwa kusoma Basmala kwa sauti katika Swala inapendeza, wakati ambapo Wanachuoni wengine wanaona kuwa kuisoma kisiri siri ni bora.

Jambo hili ni miongoni mwa sifa za Swala ambazo hazifikii kiwango cha Sunna zilizothibitishwa, kwa hiyo tofauti kuhusu suala kama hili si kubwa wala la msingi na maoni yanayolihusu ni mengi, hivyo, anayeisoma Basmala kwa sauti au yule anayeisoma kisiri siri wote wako sawa na Swala yao ni sahihi, lakini Imamu anatakiwa kutokusudia kutofautiana na watu wanaoswali nyuma yake hasa wakiwa wamezoea hali fulani kati ya sura zinazoruhusiwa kisheria.

Wala haijuzu kuwa suala kama hili liwe sababu ya kuchocheza fitina na mfarakano kati ya Waislamu, bali tunatakiwa kuwajibika kwa adabu za kutofautiana kama walivyokuwa wakifanya wahenga wetu wema ambao walikuwa wanatofautiana katika masuala ya Kifiqhi wakiwa wakiheshimiana na kupendana.

Share this:

Related Fatwas