Kuomba dua baada ya Tashahhud ya mwisho katika Swala
Question
Ni ipi hukumu ya kuomba dua baada ya Tashahhud ya mwisho katika Swala?
Answer
Kuomba dua baada ya Tashahhud ya mwisho ni Sunna iliyotoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W), nayo inapendekezwa, sio wajibu, na ana haki ya kuomba kwa lolote analotaka katika mambo ya Akhera na dunia, na ana haki ya kuomba dua zilizosimuliwa, na ana haki ya kuomba na dua nyingine. Na miongoni mwa dua zilizosimuliwa ni zile zilizopokelewa kutoka kwa Sheikh Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Aisha, (R.A), kwamba Mtume, (S.A.W), alikuwa akiomba dua katika Swala akisema: “Ewe Mola wangu, najilinda kwako kutokana na adhabu za kaburi, na kutokana na shari ya fitna ya Masihi Dajjal, na kutokana na fitna ya uhai na mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na dhambi na deni.”