Kuunga udugu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuunga udugu

Question

Ipi namna ya kuunga udugu?

Answer

Kuunga udugu ni miongoni mwa hali za Uislamu za kuimarisha muungano katika jamii; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu” [Annisaa:1].

Mtume S.A.W. amebainisha kwamba kuunga udugu na kuwafanyia wema ndugu na kuwapenda malipo yake ni Baraka katika umri na riziki; Mtume S.A.W. anasema: “Apendaye kukunjuliwa riziki yake au abarikiwe katika umri wake basi amuunge ndugu yake”.

Na sharia imemkemea mwenye kukukata udugu, na imeeleza kuwa hilo ni katika sifa za zama kabla ya Uislamu na kujiweka mbali na dini ya Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu anasema: “Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?” [ Muhammad:22]. Hivyo basi, kuunga udugu ni wajibu.

Na kuunga udugu hakuishii katika kutembeleana tu, bali kwa mambo mengine mengi kama kupeana zawadi, mawasiliano, kutumiana ujumbe na mengineyo.

Kuunga udugu si tu kwa kulipiziana wema, bali kudumu katika udugu pasi na kusubiri kitu kwa mmoja, kama alivyoeleza Mtume S.A.W.: “Si mwenye kuunga udugu mwenye kulipa, lakini mwenye kuunga udugu ni ambae ukikatika udugu wake huunga”.

Share this:

Related Fatwas