Wakala wa kisharia
Question
Ni ipi hukumu ya mteja kuweka wakala katika manunuzi ya malipo kwa awamu?
Answer
Kumuweka wakala mtu kumnunulia bidhaa mtu mwingine si vibaya; kwa mujibu wa hukumu ya uwakala ambayo ni kujuzu.
Ama mnunuzi wa bidhaa “wakala” kujiuzia mwenyewe baada ya kununua kwa uwakala; haya ni masuala wanazuoni wametofautiana katika kauli mbili; na fatwa iliyotolewa ni kujuzu wakala kujiuzia mwenyewe akipata idhini ya aliyemuwakilisha, kinyume na hivyo hakujuzu, haya ni madhehebu ya Maliki na Hanbal, na mtazamo wa madhehebu ya Shafy, na sheria ya biashara nambari 17 ya mwaka 1999, iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria nambari 168 ya mwaka 2000 na 150 ya mwaka 2001 katika kifungu (150). imechukua hili.
Ama kulipa thamani ya bidhaa kwa awamu ambayo amejiuzia wakili mwenyewe baada ya kuongeza faida iliyowafikiana, hakuna ubaya kisharia; hilo ni kwa sababu limepitishwa kisharia” kwamba kunasihi kuuza kitu kwa bei ya moja kwa moja na kwa awamu kwa muda maalum”, na kuongeza thamani kwa sababu ya muda kunajuzu kisharia kwa madhehebu yote ya fiqhi; na hii ni aina ya kuuza kwa kulipa kwa awamu.