Vazi la kisheria:
Question
Ni ipi sifa ya vazi la kisheria kwa mwanamke wa Kiislamu?
Answer
Imethibitishwa kisharia kwamba Hijabu ni katika nyajibu za kisharia, na jambo hili limekuja katika Qurani tukufu katika kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao)[An-Nuur: 31], na vazi la kisheria linalotakiwa kwa mwanamke wa Kiislamu, ni kila vazi lisilo onyesha maeneo yenye mvuto katika mwili wa mwanamke wala halionyeshi kilichopo chini yake, na linastiri mwili wote isipokuwa uso na viganja viwili, pia miguu miwili kwa baadhi ya wanazuoni wa Fiqhi, wala si vibaya kwa mwanamke kuvaa nguo zenye rangi kwa sharti zisiwe zinavutia au kuamsha hisia, Zikifikiwa sharti hizi katika vazi lolote, basi kunajuzu kwa mwanamke wa Kiisalamu kulivaa na kutoka nalo.