Wasia unaolazimu
Question
Ni ipi hukumu ya Wasia unaolazimu?
Answer
Wasia unaolazimu ni sehemu ya mali ya urithi kwa wanaostahiki kwa njia ya wasia kwa mujibu wa kanuni, sawasawwarithi wamekubali au wamekataa wasia huo. Nao ni wa watoto wa tawi la warithi wa marehemu katika maisha yake ya uzima, na kwa sharti wasiwe warithi katika asili, nalo ni wajibu kabla ya kugawa mali.
Na wasia ni wajibu na haujakatazwa kisharia; baadhi ya wanazuoni Fiqhi na wanajitihada wamepitisha, miongoni mwao nia Imamu Al-Tabary na Ibnu Hazm na Dowoud, na wametegemeza hilo katika kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: (Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wachamngu). Na hii ni kwamba aya hii inafanya kazi huku yake na haikufutwa.
Na hakuna ubaya sharia kuweka jambo ambalo linaunga undugu na maslahi ambayo hayakatazwi na nassi za kisharia, bali kuna amabazo zinatolea ushahidi.