Ustahmala
Question
Nini maana ya ustahmala
Answer
Mtumie S.A.W. alikuwa kigezo chema katika ustahmala, na walioongoka wakafuata njia yake kwa muda wote na sehemu yoyote, na hili limedhihirika katika tabia za Mtumie S.A.W. katika maisha yake matukufu kabla ya kuhamia Madina, na baada ya kuhamia Madina ikawa ndio mfumo mkuu na katiba ya mji huo na msingi mkubwa na mahusiano ya kitabia, na kanuni zinazoongoza kuanzia Siku ya kwanza Mtume alipoingia Madina yenye nuru, akianza kwa kulingania amani, ushirikiano, kuishi kwa pamoja na kuimarisha misingi ya uraia.