Duwa mvua inaponyesha
Question
Je, kuomba dua inaponyesha mvua, dua inajibiwa?
Answer
Kuomba dua mvua inaponyesha, dua inajibiwa; kipindi hicho ni katika vipindi vya kutoa na fadhila na huruma ya Mola, na Rehma za Mwenyezi Mungu Kwa waja wake; kama Hadithi ya Mtume S.A.W. inavyojuhlisha Hilo, kutoka kwa Saad R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W.: "Dua mbili hazirudi: Dua wakati wa adhana, na mvua inaponyesha".
Na kutoka kwa Abou umama R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W.: "Milango ya mbingu hufunguliwa, na Dua hujibiwa katika sehemu nne: Wakati wa kusimama mstarini katika jihadi, wakati mvua inaponyesha, na wakati wa kukimiwa Sala, na unapoiona Alkaaba" imepokelewa na Al-Bayhaqy na Al-tabarany.