Hukumu ya kufunga siku ya ishirini na saba mwezi wa Rajabu
Question
Ni nini hukumu ya kufunga siku ya ishirini na saba mwezi wa Rajabu?
Answer
Hakika kufunga saumu ya kujitolea siku ya ishirini na saba mwezi wa Rajabu ni jambo lisilo na pingamizi lolote kisheria, bali ni miongoni mwa mambo yanayopendekezwa katika siku hiyo kutangaza furaha na kuitakasa siku hiyo, kwa dalili ya kauli yake Mtume (S.A.W.): “anayefunga siku ya ishirini na saba mwezi wa Rajabu, Mwenyezi Mungu Anampa malipo ya kufunga miezi sitini”. Ingawa hadithi hiyo ina udhaifu, lakini huzingatiwa ni hadithi mojawapo hadithi za amali njema kama walivyosema wataalamu wa Fiqhi.
Pia, matini kadhaa kutoka kwa wanafiqhi wengi kusisitiza kupendekeza kufunga saumu siku hiyo kwa fadhila zake na kwa kuwa imeshuhudia tukio la pekee katika historia ya umma wa kiislamu, na kwa kuwa ni siku mojawapo siku bora zaidi ambazo saumu hupendekezwa; miongoni mwa wanazuoni hao Imamu Abu Hanifah kutokana na Imamu Al-Qarafy katika kitabu cha “Al-Dhakhirah” (2/532), Imamu Ibnu Habib na wengineo kama ilivyotajwa katika “Al-Tawdih” (2/461), Imamu Al-Ghazaly, na Imamu Al-Hattab, bali baadhi yao walitaja kuwa kufunga saumu siku hiyo ni sunna kama vile mtaalamu Suleiman Al-Gamal katika kitabu chake cha kueleza zaidi kwa kitabu cha kueleza “Manhajul-Tullab” (2/249), na mtaalamu Shata Al-Domyaty katika kitabu cha “Iantul-Talibiin” (2/306).