Tafauti kati ya elimu ya Falaki na elimu ya nyota
Question
Ipi tafauti kati ya elimu ya Falaki na elimu ya nyota?
Answer
Katika Sharia Takatifu hakuna kinachoonesha uharamu wa elimu ya Falaki au kuzuiwa, ambapo maandiko yanaonesha uovu katika elimu ya nyota (unajimu) unaotokana na dhana pamoja na kubahatisha ambapo hakufikiwi, bali hupelekea madhara kwa watu, ama elimu ya Falaki kwa kuzingatiwa ni elimu basi haipo hivyo, ambapo yenyewe ni elimu yenye weledi zake na Wasomi wake pamoja na mitaala yake, nayo ni katika elimu inayotosheleza ambayo umma wote utapata dhambi ikiwa atakosekana mtu mwenye kuijua elimu hii, kwani elimu ya falaki ina masilahi kidini na kidunia ambayo hayakamiliki isipokuwa kwa kufahamika elimu hii na kufanyika utafiti wake.