Kupandikiza vioo vya rangi vya macho
Question
Ipi hukumu ya kupandikiza vioo vya rangi vya macho kwa njia ya upasuaji?
Answer
Kufanya upasuaji ili kupandikiza vioo vya rangi vya macho ni jambo linalofaa na wala hakuna ubaya wowote kisharia, hilo ni sawa sawa likiwa ni kimatibabu kama vile kutibia uwezo wa macho kuona au kufanya hivyo kwa ajili ya pambo tu kwa sharti la kutokuwa kwa lengo la kufanya udanganyifu, na kutokuwa na madhara kwa anayefanyiwa upasuaji ni sawa sawa madhara hayo kwa hivi sasa au hata kwa siku zijazo.