Zaka ya mali ya mirathi
Question
Ipi hukumu ya Zaka ya mali ya mirathi kabla ya kupokewa?
Answer
Hakuna Zaka ya mali ya urithi isipokuwa baada ya kukabidhiwa na kupokewa pamoja na uwezekano wa kuitumia, hapo ndipo Zaka ya mali itatolewa – ikiwa masharti ya Zaka yatakamilika – baada ya kupita mwaka tokea siku ilipokabidhiwa na kupokewa hata kama itapita miaka mingi, hayo ni madhehebu ya Imamu Maliki, na pia kauli ya Imamu Abi Hanifa.