Rukia kwa kutumia Qur'ani.

Egypt's Dar Al-Ifta

Rukia kwa kutumia Qur'ani.

Question

Ipi hukumu ya Rukia kwa kutumia Qur'ani?

Answer

Rukia kwa kutumia Qur'ani Tukufu ni jambo linalofaa kwa maradhi yote, pamoja na kuchunga kuamini kuwa rukia yenyewe haiathiri, bali mwenye kuathiri ni mponyaji naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ukubwa wa huruma zake na uwezo wake, na inapaswa kuchukuwa tahadhari dhidi ya matapeli ambao wanawalaghai watu na wanachukuwa malipo kwa madai kuwa hii ni rukia.

Kilichobora zaidi ni mtu kujifanyia rukia mwenyewe au kufanyiwa na watu wema ambao uaminifu wao na uadilifu wao unafahamika.

Haya ni pamoja na angalizo, umuhimu wa kuchukuwa sababu zingine za kimatibabu ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziweka kwa viumbe wake kuwa ni sababu ya hilo.  

Share this:

Related Fatwas