Adhana ya Ijumaa

Egypt's Dar Al-Ifta

Adhana ya Ijumaa

Question

Je, Swala ya ijumaa ina adahana ngapi?

Answer

Msingi wa Adhana ya Swala ya Ijumaa ni kwamba iwe wakati wake unapoanza na Imamu anakaa juu ya mimbari, hali iliyokuwepo katika zama za  Mtume (S.A.W) na Masahaba wake, Ama kuhusu adhana nyingine, ni Sunna njema iliyowekwa na khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W), bwana wetu Othman Ibn Affan (R.A), pale watu walipoongezeka, akinuia kuwazindua ili wafanye haraka kuhudhuria kabla ya kupanda kwa Imamu juu ya mimbari, na Waislamu kwa kauli moja walikubaliana naye na limeendelea kufanyika mpaka siku hizi bila pingamizi. Imepokelewa kutoka kwa Al-Sa’ib Ibn Yazid (R.A), amesema: “Adhana ya siku ya Ijumaa mwanzo wake ni pale Imamu anapokaa juu ya mimbari katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), Abu Bakr na Omar (R.A). Ilipofika zama za Othman, (R.A), watu wakaongezeka, Adhana ya tatu ikaongezeka  kwa Al-Zawra’, na Mtume (S.A.W), hakuwa na muadhini isipokuwa  mmoja tu” (Imepokelewa kutoka kwa Imamu Al-Bukhari katika “Sahihi” yake).

Masuala hayo yenye utata yasifanywe kuwa sababu ya mgawanyiko na migogoro baina ya Waislamu, na katika suala hili, mtu lazima azingatie yale yaliyoamuliwa na mamlaka zenye uwezo wa kusimamia mambo ya misikiti.

Share this:

Related Fatwas