Kejeli kwa Wagonjwa
Question
Ni namna gani Sharia imetahadharisha kudharau na kukejeli wagonjwa
Answer
Dharau na kukejeli watu wenye msongo na matatizo ya kisaikolojia ni jambo ovu na baya Kisharia na ni uhalifu kisharia, na hilo ni kutokana na kuwepo kero na madhara, kuongezea pia hatari kwa usalama wa kijamii kwa kuwa kwake ni uhalifu, Sharia ya Kiislamu kwa hakika imekuja ili kuwahimiza watu kujipamba na tabia na maadili mema na kuwa mbali na matumizi ya kauli chafu na vitendo viovu.
Ofisi ya Mufti wa Misri inatoa wito kwa watu wa makundi yote ya jamii kufanya kazi ya kupambana na hali hiyo ili kufikia ufumbuzi wa tukio hili na kupambana nalo, taasisi za kielimu za kiulinganiaji na za habari zinapaswa kubeba jukumu lake kupitia kuelimisha juu ya hatari ya kitendo hiki kwa kuelimisha utamaduni wa kutakana radhi ndani ya jamii na kuchunga haki za wengine.