Sanamu la kumbukumbu na sanamu la askari asiyefahamika.
Question
Upi msimamo wa Uislamu katika sanamu la kumbukumbu na la askari asiyefahamika?
Answer
Kuwakirimu mashahidi waliofariki kwa kuwatengenezea kinachofahamika kama “sanamu la kumbukumbu” ni jambo halali Kisharia, na linaingia katika ujumla wa maandiko ambayo yanathibitisha ukubwa wa nafasi mbele ya Mwenyezi Mungu ya mtu aliyefariki kama shahidi, kama ilivyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapo pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!} An-Nisaa: 69.
Watu mashahidi siku zote wanakuwa kwenye akili za Umma, ambapo hawasahuliki kwenye kumbukumbu na akili za watu wao, mpaka ufahamike ukubwa wa nafsi yao mbele ya Mwenyezi Mungu na watu kufahamu makubwa waliyoyafanya kwa ajili ya nchi yao, ili kuimarisha msingi wa uaminifu kwa nchi, na ukiwa ni utekelezaji wa yale yaliyokuja ndani ya Qur`ani Tukufu katika kuwakirimu na kuimarisha kudumu kwa uhai wao na kubakia kwa muda mrefu roho zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni hai,wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi * Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika * Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini} Aal-Imran: 169 – 171.