Swala ya kuamkia Msikiti wakati wa hotuba ya Ijumaa.
Question
Je, kunajuzu kuswali swala ya kuamkia Msikiti wakati hotuba ya Ijumaa ikiendelea?
Answer
Kuswali rakaa mbili za kuamkia Msikiti pindi mwenye kuswali akiwa amefika Msikitini na hotuba ya Ijumaa inaendelea ni jambo lenye kauli tofauti kati ya Wanachuoni, kwa vile ni jambo lenye kauli tofauti basi mwenye kuziswali hizo rakaa mbili atakuwa amekubaliana na jitihada iliyosahihi, wala hakuna yeyote anayempinga mwingine kwenye hilo, kwa sababu jambo lenye tafauti halipingwi.