Daishi ni kundi la kihalifu la umwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Daishi ni kundi la kihalifu la umwagaji damu lisilo halali

Question

Je, Daishi ni kundi halali linalozungumza kwa jina la Uislamu?

Answer

Daishi ni kundi la kihalifu la umwagaji damu ambalo halina uhalali wowote kwa jina la dini ya Kiislamu, bali Uislamu unaharamisha matendo yake na kuwatishia wahusika wake adhabu kali duniani na Akhera.

Hii ni kwa sababu Uislamu ni dini ya amani, usalama, na rehema kwa walimwengu. Kamwe haukuegemea kwenye umwagaji damu na kuwatisha watu wanaoishi salama, jambo ambalo ni kinyume na kile kinachofanywa na Daishi kwa kufikia madai ya ukhalifa kwa mtazamo wao ambao hauwiani kamwe na madhumuni ya Sharia katika nukta kadhaa:

1- Dhana ya ukhalifa yenyewe imebadilika na kustawi tangu zama za Ukhalifa Ulioongoka hadi leo. Kwa kupita karne na karne na kupanuka kwa Uislamu na kuongezeka kwa idadi ya Waislamu, hakuna tena khalifa anayetawala ulimwengu wa Kiislamu peke yake. Hivi sasa kila nchi au ufalme umekuwa na Imamu fulani au Sultani au Raisi.

2- Utumiaji wao wa kikatili na potofu wa dhana ya jihadi kwa uadui dhidi ya serikali zinazotawala, kuua Waislamu wasio na hatia, kuwateka wanawake wao, na kuchukua pesa zao kwa dhulma na kwa fujo, na nchi zilizotawaliwa na Daishi ni mashahidi wa uhalifu huu.

3- Makosa yanayofanywa na Daishi yanazingatiwa kuwa ni ufisadi katika ardhi bila ya haki ambayo inalazimu utekelezaji wa adhabu ya kuikata njia, Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha au watolewe katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah watapata adhabu kuu}

Share this:

Related Fatwas