Kukaa vikazi vya kumtaja Mwenyezi Mungu Msikitini
Question
Ipi hukumu ya kukaa vikazi vya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtikitini?
Answer
Kukaa vikazi vya kumtaja Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu ndani ya Misikiti na maenezo mengine – baada ya kupata kibali husika – ni katika ibada za Kisharia, na zinakubaliana na yaliyokuja ndani ya Kitabu na Sunna pamoja na uongofu wa waja wema waliotangulia na Wanachuoni wa umma, kwa sharti la kuchunga adabu za Kisharia na mifumo ya maeneo.
Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa sauti katika makazi haya pamoja na kuchunga adabu zilizotajwa ni jambo linalokubalika pia, ambapo iwe kwa sura isiyoleta ushawishi kwa wanaoswali na wanaomtaja Mwenyezi Mungu pamoja na wasomaji wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hilo ni kufuata maelekezo ya Mtume S.A.W katika kauli yake:
“Msipandishiane sauti nyinyi kwa nyinyi kwa kusoma Qur'ani”