Mitazamo ya Turathi za zamani na athari za shani hii katika kuenea kwa ugaidi
Question
Je! Kuhamasisha Mitazamo ya Turathi za zamani kunaendana na uhalisia wa sasa? na zipi athari za shani hii katika kuenea kwa ugaidi?
Answer
Uhalisia una athari yake kubwa katika kutengeneza Fiqhi na Fatwa za kisheria, na hii ni sababu moja kubwa ya kwenda kwa hatua katika Sharia, kwa mfano tunakuta Swala mwanzoni ilipofaradhishwa sio kama ilivyokuwa mwishoni kipindi cha Mtume S.A.W. imepokewa Hadithi kutoka kwa Abdullah bin Masoud R.A. amesema: Tulikuwa tunamsalimia Mtume S.A.W. akiwa katika Swala, na anaitikia salamu, tuliporudi kutoka kwa mfalme Al-Najashy tulimsalimia hakuitikia salamu, na akasema: “Hakika katika Swala kuna shughuli”[Imekubaliwa na wote]. Miongoni mwa matatizo ya wanaofuata itikadi kali, ni kwamba hawachungi hali halisi, na wanachukulia kuwa kila tukio lililo kinyume na ilivyokuwa zama alizoishi Mtume S.A.W. basi hilo ni tukio baya, na wanajaribu kulibadili kwa njia mbalimbali, na Maimamu wa turathi hawakufanya hivyo, na walienda kinyume na waliowatangulia katika mambo mengi ili kuchunga hali zao, na vitabu vyao vimejaa hayo, wajibu wetu ni kuwafuata na kuchunga hali zetu, na tusiache jitihada zao kwa sababu ya hali zetu kama ilivyo, na hii ndiyo duru ya Wanazuoni wenye kubobea.