Hatari ya watu wa kawaida wanaouliz...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hatari ya watu wa kawaida wanaouliza Fatwa kuomba dalili kutoka kwa Mufti

Question

Ni ipi hatari ya watu wa kawaida wanaouliza Fatwa kuomba dalili kutoka kwa Mufti?

Answer

Mtu wa kawaida asiyebobea katika elimu ya kisharia kumtaka Mufti dalili katika Fatwa kumekatazwa, hilo ni kwa sababu mtu asiyebobea si mtu wa kuangalia dalili, na anaweza ikawa dalili yenyewe haielewi au anaielewa ndivyo sivyo, na huko ni kupoteza muda na juhudi au kueneza ujinga, na yote hayo yanakemewa na Sharia, mtu anayetaka Fatwa akimwuliza Mufti idadi ya rakaa za Adhuhuri kwa mfano, akamwambia ni rakaa nne, akamtaka dalili, akamwambia ni Ijmaa  (makubaliano ya Wanazuoni), anayeuliza atataka kujua maana ya Ijmaa, na ni ipi hoja yake, na ipi dalili ya hoja yake? Na aina zake ni ngapi? Na Ijmaa hii ipo katika aina gani? Na hili ni somo kubwa katika elimu ya Usuul Fiqhi (Misingi ya Fiqhi) na sio wote wanalielewa, na lazima liwe na utangulizi, na hivyo tunakuta kwamba Maimamu wameelezea hapo zamani, kwamba hakufai kwa anayetaka Fatwa kumwomba Mufti dalili ya Fatwa yake, lakini akitaka basi asome, ijapokuwa kwa kiasi cha kutuliza nafsi yake, hapo anaweza kukubali au kukataa Fatwa.

Share this:

Related Fatwas