Mifano minne ya hali ya Muislamu akiwa anatendeana na watu wengine.
Question
Ni ipi mifano minne ya hali ya Muislamu akiwa anatendeana na watu wengine?
Answer
Kwa hakika, Mtume (S.A.W.) ametuachia katika Sunna zake mifano minne ya miamala ya Muislamu na watu wengine; mfano wa kwanza, ni mfano wa hali ya Waislamu walipokuwa Makkah, ambapo Muislamu alikuwa akiishi katika nchi ya watu wanaopinga Uislamu na kupigana vita na Waislamu, hapo Muislamu alikuwa na subira na uvumulivu mkubwa wakiishi kwa amani.
Mfano wa pili ni mfano wa Waislamu waliokuwa Wakiishi Uhabeshi, ambapo Waislamu walikuwa wakiishi na watu ambao hawakupigana nao ingawa hawakujiunga na Uislamu, katika mfano huu Waislamu walishirikiana na wenzio katika nchi kwa msingi wa kuheshimiana.
Mfano wa tatu nao ni mfano wa jamii ya Madinah katika siku zake za mwanzo, ambapo Waislamu waliishi katika nchi yenye wafuasi wa dini, madhehebu na makabila tofauti tofauti, hapo ndipo jamii hiyo ilikuwa ni jamii ya kukamilishana na kusaidiana kwa wote.
Mfano wa nne ambayo ni mfano wa jamii ya Madinah katika siku zake za baadaaye ambapo Waislamu walikuwa wengi zaidi wakilazimika kwa misingi ya uadilifu na uelewa wa mambo kabla hawajafanya lolote, kwa jumla hali ya Muislamu kulingana na kuishi na kuingiliana na jamii yake haina budi kuwa katika mfano mojawapo ya mifano hiyo minne.