Jihadi katika Uislamu ni ya kujitetea au ya kuanza adui
Question
Tukimaanisha kwa istilahi Jihadi kupigana, basi mapigano haya ni ya kujitetea au ya kuwashambulia?
Answer
Jihadi kwa maana ya mapigano katika Uislamu ni Jihadi ya kujitetea siyo Jihadi ya kuanza uadui dhidi ya wengine, anayesoma sunna za Mtume kwa makini hutambua vema kuwa Jihadi imefaradhishwa baada ya kuhama kwa Mtume (S.A.W.) na kwamba Waislamu walibaki miaka kadhaa Makkah wakiteseka na kudhulumiwa kwa maudhi na adhabu walizofanyiwa na washirikina wa Qureish wakitakiwa kuvumulia na kutaka malipo ya subira na uvumulivu huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mpaka Mtume (S.A.W.) akawaruhusu kuhama kwenda Uhabeshi kwa kuongozeka kwa mateso na uadui, kisha Mwenyezi Mungu (S.W.) Akamteremshia Mtume wake (S.A.W.) kauli yake: {Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia} [Al-Hajj: 39], anayefikiria Aya hii Tukufu huelewa kuwa sababu ya kuruhusu mapigano ni kuondoa dhuluma na uadui wanaofanyiwa Waislamu, kisha Mwenyezi Mungu Akawafaradhishia Waislamu kupigana vita, ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui} [Al-Baqarah: 190], Aya hii iko wazi kuwa walengwa kwa mapiganao ni wale wanaowapiga Waislamu tu, sawa sawa uadui wao huu ulikuwa kwa sababu ya kupigana dini au kwa makusudio mengine ya dunia kama vile kupora mali za umma.