Aliyekufa hali ya kuwa ni tajiri n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Aliyekufa hali ya kuwa ni tajiri na hakuhiji

Question

Ni ipi hukumu ya aliyekufa hali kuwa ni tajiri na hakuhiji?

Answer

Inapendekezwa kwa mtu ambaye ana uwezo wa kifedha na kimwili afanye haraka kutekeleza Hijja ya Faradhi, na inajuzu kwake kuichelewesha ikiwa anadhani kuna uwezekano mkubwa wa kuwa salama, na akidhani kuwa atakufa kutokana na kuoneka na maradhi au uzee, basi ni lazima atekeleze Faradhi hiyo mara moja.

Iwapo alikuwa na uwezo wa kutekeleza Hijja ya Faradhi na akafa kabla ya kuitekeleza, basi ni lazima awe amekufa hali ya kuacha wasia na ana urithi. Hijja itatekelezwa kwa niaba yake kwa njia ya wajibu kutoka katika theluthi moja ya mali yake, au alikufa bila ya kuacha wasia na alikuwa na mali, basi si wajibu kwa warithi wake kuhiji kwa niaba yake, bali ni jambo la kupendekezwa, na hali hiyo hiyo inatumika kwa mtu aliyekufa na hakuwa na mali na hakuacha wasia.

Share this:

Related Fatwas