Israa na Miiraji.
Question
Upi ukweli wa muujiza wa Israa na Miiraji, na ipi dalili ya kutokea kwake, na ipi hukumu ya mwenye kuupinga?
Answer
Safari ya Israa na Miiraji ni tukio limetokea kweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na limemtokea akiwa macho kwa kupewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuinua uwezo wake, ambapo Mtume S.A.W alikwenda safari hii usiku akiwa macho kutoka Msikiti Mtakatifu wa Makka na kwenda Msikiti wa Al-Aqsaa, aliwaswalisha Malaika na Manabii Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwao wote kisha akapandishwa akiwa macho kutoka Msikiti wa Al-Aqsaa na kwenda mpaka mbinguni, na kutoka huko mbinguni akafika mpaka sehemu ya juu zaidi.
Mtume S.A.W ndani ya usiku huo uliobarikiwa alioneshwa alama nyingi takatifu, miongoni mwazo: Pepo, ili apate kuona yale yaliyoandaliwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wake miongoni mwa malipo na neema ili apate kuwabashiria wacha-Mungu, vile vile Mtume S.A.W alioneshwa moto ili apate kuona yaliyoandaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu wake ikiwa ni pamoja na adhabu kali, ili apate kuwaonya nayo makafiri na washirikina.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya usiku huo akampa Mtume wake S.A.W ibada ya Swala tano aziswali usiku na mchana katika malipo zinakuwa sawa na Swala hamsini, na akahusishwa kupewa jambo kubwa wasiopewa yeyote katika ndugu zake Manabii Amani iwe kwao wote.
Yameelezwa hayo kwenye Qur`ani na Hadithi pamoja na Maswahaba na Wanachuoni, haya ni katika yasiyopaswa kwa yeyote kuyakana, na hakuna anayeyapinga isipokuwa wakiukaji wenye kujikweza.