Usafirishaji wa vitu vya kale
Question
Nini hukumu ya kuuza vitu vya kale au vitu vingine vinavyopatikana, na kuvifanyia biashara kwa ujumla?
Answer
Hairuhusiwi kisharia kuvifanyia biashara kwa vitu vya kale kwa kuviuza, kuvifanya zawadi, au kwa njia nyinginezo, isipokuwa ndani ya mipaka ya kile kinachoruhusiwa na mwenye mamlaka na kudhibitiwa na sharia kwa njia ambayo inafanikisha masilahi ya umma, mtu akivipata kwenye ardhi anayomiliki. Uhamisho wa umiliki wa ardhi hauhusishi uhamishaji wa umiliki wa vitu vya kale vilivyozikwa katika ardhi hiyo, isipokuwa mmiliki wa sasa ni mmoja wa warithi wa mmiliki wa kwanza wa mali iliyozikwa – hali ambayo haiwezekani - lakini umiliki haujathibitishwa hata ikithibitika kuwa yeye ni mmoja wa warithi wa mmiliki wa kwanza; Kwa mazingatio mengi, na ikiwa umiliki wa vitu vya kale haujahamishiwa kwa mmiliki wa sasa kwa njia hii, basi vitu vya kale vile ni pesa za umma, na vinakuwa viokotwa ambavyo lazima virudishwe serikalini, na hii ndio inayofanywa katika nchi ya Misri katika Fatwa na Mahakama.
Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.