Jihadi iliyopo katika vitabu vya zamani
Question
Je, fiqhi ya Jihadi iliyopo katika vitabu vya zamani huzingatiwa msingi mojawapo misingi ya sheria ama ni fiqhi inayokubali kubadilika?
Answer
Fiqhi ya Jihadi iliyopo vitabu vya zamani iko katika sehemu ya Fiqhi inayokubali kubadilika kwa jitihada za wataalamu, ambapo hapana hukumu iliyo thabiti bila ya mabadiliko isipokuwa hukumu ya msingi ya kuruhusu Jihadi, kwani ilithibitishwa kuwa njia ya kujibu dhuluma ya dhalimu na uadui ya wafanyao uadui kwa dalili ya Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume (S.A.W.), Mwenezi Mungu (S.W.) Amesema: {Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia} [Al-Hajj: 39], na katika Sunna Hadithi iliyosimuliwa kuwa "Mtume (S.A.W.) aliulizwa: ni nini kazi iliyo bora? Akajibu: Kumwamini Mwenyezi Mungu na kufanya Jihadi kwa ajili yake" [imekubaliwa na wote], ikumbukwe kuwa hukumu ya kuruhusu Jihadi huambatanishwa na masharti yaliyokubaliwa na wanafiqhi ambayo ni sawa sawa na misingi ya kisheria kama vile; uwepo wa Imamu na kupata ruhusa yake, lakini hukumu ndogo ndogo za Jihadi zinazohusiana na aina zake, ambazo ni sehemu kubwa ya hukumu za Jihadi, basi ni hukumu zinazobadilika badilika kutokana na kubadilika kwa hali na wakati, kwa mujibu wa maoni ya mtawala na sera zake nzuri.