Hadithi: “Kundi la umma wangu litae...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hadithi: “Kundi la umma wangu litaendelea kushikamana na haki.”

Question

Watu wengi wenye misimamo mikali huegemeza mashambulizi yao kwa watu kwenye Hadithi: “Kundi la umma wangu litaendelea kushikamana na haki.” Je! Hadithi hii ni sahihi? Na ina maana gani?

Answer

Hii ni moja ya Hadithi ambazo baadhi ya wakufurishaji huzitumia kama ushahidi wa kuhodhi haki, na hivyo kudhalilishwa huku kwa watu, matokeo ya kutokuelewa na kutoka kifikra katika mfumo wa kisharia ambao Maimamu waliuainisha ili kuelewa dhamira ya Utume kutokana na Hadithi zilizopokelewa kuhusu suala hili.

Hadithi hiyo ni sahihi bila shaka, na imekuja katika hali ya kujulisha juu ya Sunna ya ulimwengu ambayo itatokea bila shaka, na sio kuanzishwa na kikundi au madhehebu, na hairuhusiwi kwa madhehebu au kikundi kuhodhi jina au sifa ambayo imeelezwa kwenye kundi hilo, Mtume (S.A.W.) hataki kuifafanua, bali anataka tujitahidi kufikia sifa hizi ndani yetu, licha ya maovu iwapo kila mwenye mwenye kudai anadai kitu asichokuwa nacho, basi watu wanakuwa makundi na madhehebu mengi, kila mmoja akidai mtazamo wake na ufahamu wake. Inawezekana kundi hili imegawanyika baina ya aina za waumini, baadhi yao ni wapiganaji mashujaa, baadhi yao ni Wanachuoni wa Fiqhi, baadhi yao ni Wanachuoni wa Hadithi, na baadhi yao ni Wanachuoni, wanaamrisha mema na wanakataza maovu, na baadhi yao ni watu wa aina nyingine wa matendo mema, si lazima wawe pamoja, bali wanaweza kutawanyika katika sehemu zote za ardhi. Hadithi imekusudiwa kutuhimiza tuwe miongoni mwa watu wa haki na tusihodhi haki.

Share this:

Related Fatwas