Hadithi: "Nilitumwa na upanga"
Question
Watu wengi wenye misimamo mikali huegemeza mashambulizi yao kwa watu kwenye Hadithi: “Nimetumwa kwa upanga.” Je, Hadith hii ni sahihi? Na ina maana gani?
Answer
Hadithi hii ilipokelewa kwa mapokezi mengi, na nguvu zake zimekusanywa kutoka kwenye wapokezi wa Hadithi, na neno la: “Upanga” ni makhsusi kwa Mtume (S.A.W.) na pia yule anayechukua nafasi yake, na inawezekana kuwa Mtume (S.A.W.) alitaka kuwatisha wasiokuwa Waislamu na kuwakumbusha uwezo na ulinzi alionao kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Hadithi hii inahusiana na wajibu wa jihadi, na hapana shaka kwamba jihadi imetajwa kwake matini nyingi ya kuihimiza, lakini pamoja na hayo jihadi ina udhibiti sawa na mambo mengine ya halali, kama inavyojulikana kwa wenye elimu, kuwa jihadi ni faradhi kifaya. Mwenyezi Mungu anasema: “Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?” [At-Tawbah: 122] Inajulikana kuwa Uislamu una unazingatia sana kufikisha ujumbe wake kwa walimwengu, na jihadi ni njia tu ya ufikishaji huo. Mtazamo sahihi ni kwamba suala la jihadi linategemea kile ambacho mtawala anakiona kuwa ni wema kwa Uislamu na watu wake ikiwa ni vita au amani, siyo lazima kwa vita tu, au kwa makubaliano. Wakati usalama wa wasiokuwa Waislamu ukitokea kutoka kwa mtawala au mtu mwingine yeyote kwa masharti maalumu, lazima Waislamu wote watimize. Hairuhusiwi kukamata au kuchukua chochote kutokana na fedha zao isipokuwa kwa njia ya halali, wala kukabiliana nao bila ya njia ya kisharia.