Udhaifu wa kufahamu elimu ya Sharia...

Egypt's Dar Al-Ifta

Udhaifu wa kufahamu elimu ya Sharia.

Question

Ipi nafasi ya udhaifu wa kufahamu elimu ya Sharia katika kutengeneza akili ya ukufirishaji?

Answer

Ujinga ndio mazingira sahihi ya kueneza fikra za misimamo mikali, kwa sababu fikra za misimamo mikali ni fikra za juu  juu zinategemea dalili za kuteua na tafsiri ya juu juu ya maandiko ya Kisharia, hivyo kazi za mafunzo ya kijeshi siku zote huathiri wenye maarifa madogo ya elimu ya dini na Sharia kwa kukosa uwezo wa kuchambua mafundisho ya misimamo mikali, na kufahamu pingamizi zake na udhaifu wake, mara nyingi hiko ndicho kinachoonekana katika takwimu za kiwango cha maarifa ya elimu ya Sharia kwa wapiganaji wa vikundi vya misimamo mikali.

Hivyo wananadharia wa fikra za misimamo mikali wanafanya juhudi za kuimarisha ujenzi wa uelewa mpya unaohudumia mitazamo ya misimamo mikali ambayo wanaifanyia juhudi katika kuihudumia, kutokana na hilo jambo la kwanza mtu anagongana nalo anayeanza kusoma matokeo ya fikra za watu wa misimamo mikali au kufuaatilia rekodi zao na vitabu vyao, ni mkusanyiko wa uelewa ambao umekuwa ni jengo la kifikra za mfumo huo, wanaeleza maana ya “Nchi ya kikafiri na nchi ya Kiislamu” kwa maana ya Sayyid Qutwub na wengine, ili kusisitiza kuwa jamii yake ni jamii ya kijinga, na nchi yake ambayo anaishi ni nchi ya kikafiri wala si ya Kiislamu, na kuelezea “Mambo ya Utawala”  na namna gani utawala wa Kiislamu unavyokuwa, ili kumkinaisha kabisa kuwa mifumo ya utawala ni mifumo ya kikafiri, na yule mwenye kuisaidia anashiriki katika huo utawala, kisha wanafundisha jihadi na njia ya kuitekeleza, ili kuhamasisha kuuwa raia Waislamu na watu wengine wa dini zingine, hivyo hupelekea ujenzi huo wa maana mpya kutekeleza kazi zake za kumuhamasisha mtu huyo kuelekea kwenye misimamo mikali.

Share this:

Related Fatwas