Kudanganya katika bidhaa zilizokuba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kudanganya katika bidhaa zilizokubaliwa kutolewa

Question

Je, ni ipi hukumu ya kudanganya bidhaa zilizokubaliwa kutolewa katika zabuni?

Answer

Kudanganya katika bidhaa zilizokubaliwa kutolewa katika zabuni na zinazofanana na hizo ni haramu kwa mujibu wa Sharia, na ni kula pesa kinyume cha Sharia. Uislamu umeharamisha kudanganya na hadaa, Mtume amesema: “Atakaetuhadaa si katika sisi.” Imepokelewa kutoka kwa Al-Darimi na asili yake ni katika vitabu viwili vya Sahihi. .

Kadhalika Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waislamu kuwa waaminifu na kuwa pamoja na wakweli. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli} [At-Tawbah: 119].

  Uislamu pia unalazimisha utimilifu wa masharti maadamu hauvunji sharia au matakwa ya mikataba. Mtume (S.A.W) amesema: “Waislamu washikamane na sharti zao, isipokuwa kwa sharti inayoharamisha kinachoruhusiwa au kuruhusu kilichoharamishwa.” Imepokelewa kutoka kwa Al-Daraqutni.

Share this:

Related Fatwas