Mashaka katika jambo lililowekwa na...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mashaka katika jambo lililowekwa nadhiri

Question

Mtu mmoja aliweka nadhiri kisha akatilia shaka nadhiri hiyo. Nini hukumu yake?

Answer

Mwenye kuweka nadhiri basi akatilia shaka au akasahau aina ya nadhiri aliyoiweka; Je, ni Swala, au kufunga Saumu, au kutoa Sadaka, au kitu kingine? Anajitahidi mpaka afikiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa ni mfano wake, na anafanya hivyo. Na akijitahidi na aina ya nadhiri haikubainika kwake, ni wajibu atoe kafara ya viapo. Kwa sababu shaka juu ya lililowekwa nadhiri ni kama kutolitaja, na kwa sababu kutoweza kwake kubainisha aina ya nadhiri ni sawa na mtu aliyeweka nadhiri kisha akashindwa kuitekeleza.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas