Kuadhimisha maadhimisho mbalimbali ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuadhimisha maadhimisho mbalimbali ya kidini

Question

Ipi hukumu ya maadhimisho mbalimbali ya kidini kama vile kuadhimisha usiku wa Lailatul Qadri, Israai na Miiraji, mazazi ya Mtume na mengine?

Answer

Maadhimisho ya minasaba ya kidini ni jambo lenye kupendeza halali hayachukizi wala si uzushi, bali ni katika kutukuza alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo} Al-Hajj: 32. Maadhimisho haya ni katika athari za kinafsi na kimalezi kwa watu ambapo manufaa yake yanarejea kwenye kuthibitisha utaifa na dini katika nafsi zao, na kukusanyika kwa ajili ya hayo maadhimisho ni katika kujenga mawasiliano na wema wenye kuondoa shari nyingi ambazo zinakuja kutokana na upweke na kujitenga, na kupatikana manufaa yanayohitajika sana na jamii, nayo pia ni nafasi au fursa ya kulisha chakula na kueneza amani na kuunganisha undugu.

Sharia Takatifu imekuja na amri ya kukumbuka masiku ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake:

{Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu} Ibrahim: 5. Na imekuja Hadithi ya Mtume S.A.W anasema:

“Hakika katika masiku ya Mola wenu Mtukufu kuna masiku bora yenye baraka, hivyo zitumieni kwa maombi, kwani huenda mmoja wenu akizipata hizo baraka hatupatwa na ubaya kabisa”

Katika umaalumu wa uhalali wa maadhimisho ya kumbukizi ya mazazi ya Mtume S.A.W vile vile na kuteremshiwa wahyi, imepokewa Hadithi na Imamu Muslimu kuwa Mtume S.A.W aliulizwa kuhusu kufunga siku ya Jumatatu akasema:

“Hiyo ni siku niliyozaliwa, na siku niliyopewa Utume – au kuteremshiwa wahyi -

Share this:

Related Fatwas