Kuzungumza katika mambo ya tiba pas...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuzungumza katika mambo ya tiba pasi na elimu

Question

Ni ipi hukumu ya kuzungumza katika mambo ya tiba kwa watu wasiobobea?

Answer

Kumuandikia dawa mgonjwa ni katika kazi za madaktari, haijuzu kwa asiekuwa daktari aliebobea kuthubutu na kuzungumza katika mambo ya matibabu au kumuandika dawa mgonjwa, Mtume S.A.W. ametahadharisha mtu asiekuwa daktari kumtibu mgonjwa akiwa hana vigezo vya hilo, na akaeleza kuwa mwenye kufanya hivyo anabeba matokeo yake, wala hasamehewi kwa nia njema, Mtume S.A.W. anasema: “Mwenye kujifanya daktari na hakuwa mjuzi wa tiba; basi atabeba matokeo yake” Imepokelewa na Abu Dawoud.

Kunatakikana kwa mtu mwenye akili kutoweka jambo linalohusu afya yake kwa mtu anayefanya anajua kila kitu, kuchezea maisha ya watu na kudhuru afya zao na miili yao na kufanya hivyo ni aina ya ufisadi duniani unaopinga na matakwa ya Uislamu katika kulinda maisha ya mwanadamu na kuharamisha kumdhuru.

Share this:

Related Fatwas