Kuuza dawa zisizojulikana zinapotok...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuza dawa zisizojulikana zinapotoka

Question

Ni ipi hukumu ya Kuuza dawa zisizojulikana zinapotoka na zisizo na kibali? 

Answer

Baadhi ya maduka ya dawa huuza dawa za magendo zisizojulikana chanzo chake na hazina kibali kutoka wizara ya afya, jambo hili ni haramu kisharia; Nasi za kisharia zimekataza kudhuru nafasi na kuziingiza katika kuangamia, na zimeamrisha kuzilinda kutokana na hatari mablinbali; Mwenyezi Mungu Anasema: (Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo..) [Al-Baqara:195].

Mwanachuoni Ibnu Ashour anasema katika "Al-Tahreer wa Al-Tanwir" (215/2) Kila kinachosababisha maangamizi kwa makusudi basi ni haramu muda wa kuwa hakuna muktadha wa kuondoa uharamu huo.

Pia kusambaa kwa dawa hizo ni kumpinga kiongozi ambaye Qurani imeamrisha kumtii; Mwenyezi Mungu Anasema: (Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi)[An-Nisaa:59]; Sheria ya Misri inaeleza kupiga marufuku na ni makosa kuuza dawa zisizoruhusiwa kwa maduka ya madawa au watu wengine kama vile madalali wa kuuza dawa, kama kinavyosema kifungu namba (28) katika Sheria ya kuuzaza dawa namba (127) ya mwaka 1995.

Share this:

Related Fatwas